Thursday, 3 November 2016

SINGIDA: ENEO LA UZALISHAJI UMEME WA UPEPO NCHINI


Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Dodoma
Maeneo ya Kititimo na Kisaki mkoani Singida yametajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo mazuri nchini yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya upepo.  
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani amesemwa hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu sawali la Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa lililohoji ni lini mradi huo utaanza kuzalisha umeme huo mkoani humo.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Kalemani amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa ikifanya tafti kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo utaanza ifikapo Aprili 2017 na kutarajiwa kukamilika mwaka 2019 baada ya majadiliano kati ya TANESCO na kampuni ya Wind East Africa Ltd kukamilika mwezi Desemba 2016” amesema Naibu Waziri Kalemani.
Kupitia tafiti hizo, Naibu Waziri Kalemani amesema kuwa kampuni binafsi ya Wind East Africa Ltd yenye Wabia watatu ambao ni Six Telecoms (Tanzania), kampuni ya Kimataifa ya Aldwych ya nchini Uingereza pamoja na moja ya wajumbe wa Benki ya Dunia (IFC) ambao utagharimu jumla ya kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 264.77.
Aidha, Naibu Waziri Kalemani kampuni nyingine inayoonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa kufua umeme wa upepo ni mkoani Singida kuwa ni Geowind Ltd ambayo ipo tayari kuzalisha umeme wa Megawati 50 eneo la Kititimo ambapo kampuni hiyo tayari ina eneo la hekta 1,450, mradi huo unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 136 na kukamilika mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment